Saturday 28 January 2017

Vijana wawili waweka rekodi kwa kufunga ndoa rahisi isiyokuwa na mbwembwe.

Wanaume wengi tunapenda kufunga ndoa za gharama nafuu lakini wenza wetu ukiwapa mkakati huo wanageuka mbogo na kuwa wachungu kama shubili. Sasa ebu tuchukue somo kupitia vijana hawa kutoka nchini Kenya.

Vijana wawili wapenzi ambao stori yao kuhusu ndoa ya bei rahisi waliyofunga ilizua hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii, sasa wameahidiwa kulipiwa gharama zote za mapumziko baanda ya ndoa (honeymoon).


MUTURA3-750x375.jpg

Wilson Mutara (26) na Ann Wambui (24) kutoka nchini Kenya inaripotiwa kuwa walifunga ndoa kwa gharama ya Ksh 100 ambayo ni sawa na TZS 2,147 ambapo gharama hizo zilikuwa kwa ajili ya kununua pete tu.


C3J9guVVUAAGPN0.jpg

Ndoa hiyo iliyotajwa kuwa ya bei rahisi kuwahi kutokea nchini humo haikua na sherehe baada ya wawili hao kutoka kanisani na walivalia fulana walipokwenda kufunga ndoa.

“Tulikwenda nyumbani tukapika ugali na sukuma wiki, tukala na tukalala. Hakuna kitu cha kipekee tulichokifanya katika mapumziko (honeymoon) yetu” alisema Mutura.

C3J9gzGUkAEys3K.jpg
Mchungaji aliyefungisha ndoa hiyo alichapisha habari hiyo na ndipo mwakilishi wa Kampuni ya Utalii ya Bonfire Adventure alipokutana na wanandoa hao.

C3MA8bzWIAAwt5I.jpg

Kampuni hiyo ndiyo ilijitolea kudhamini mapumziko ya wawili hao baada ya kufunga ndoa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

YouTube

Blog Archive

Pages

Our Facebook Page

Hali ya Hewa

Waliotembelea